
TANGAZO LA UTETEZI WA TASINIFU YA PhD YA DKT. JEREMIA J. PYUZA
TANGAZO LA UTETEZI WA TASINIFU YA PhD YA DKT. JEREMIA J. PYUZA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini -KCMC , kwa kushirikiana na Leiden University Medical Center (LUMC)The Netherlands, Chuo Kikuu KCMC, na Kilimanjaro Clinical Research Institute (KCRI) , inapenda kuwafahamisha wadau, wanafunzi, watafiti na jamii kwa ujumla kuhusu tukio muhimu la kitaaluma: Utetezi wa Tasnifu ya Uzamivu (PhD Defence) ya Dkt. Jeremia J. Pyuza.
Tasnifu yake yenye kichwa cha “The Immune Divide: Factors Influencing Immune Variation and Differences in Vaccine Responses”, imechunguza kwa kina sababu zinazochangia utofauti wa mfumo wa kinga na namna hali hii inavyoathiri majibu ya chanjo kwa watu mbalimbali. Moja ya gunduzi inayotokana na utafiti huu ni kwamba maisha ya kila siku yana mchango mkubwa katika mfumo wa kinga mwili na hatimaye chanjo (Soma majarida ya kimataifa yaliyochapishwa na Dr. Jeremia J Pyuza)
Utafiti huu ni mchango mkubwa katika kuboresha mbinu za kimatibabu, hasa matibabu yanayotegemea kinga ya mwili na chanjo ambazo zinamchango katika kuzuia magonjwa ya kuambukiza, na kuongeza ufanisi wa chanjo duniani kwa ujumla.
Dkt. Pyuza ametafiti chini ya uongozi wa timu ya wasimamizi wenye uzoefu mkubwa kutoka LUMC(The Netherlands) na KCMC( Tanzania), sambamba na jopo la watahini (examiners) kutoka vyuo mbalimbali vya kimataifa atafanya utetezi(defence) ya tasnifu hiyo.
Utetezi huu unafanyika:
Tarehe: 25 Novemba 2025
Muda: Saa 6:00 mchana (TZ) | Saa 4:00 asubuhi (NL)
Mahali: Academy Building, Rapenburg 73, Leiden – The NetherlandsKwa wale ambao hawawezi kuhudhuria moja kwa moja, tukio hili litarushwa moja kwa moja kupitia link hii
Tunamtakia kila la heri katika utetezi wake wa tasnifu!